unfoldingWord 25 - Shetani Anamjaribu Yesu
Muhtasari: Matthew 4:1-11; Mark 1:12-13; Luke 4:1-13
Nambari ya Hati: 1225
Lugha: Swahili
Hadhira: General
Kusudi: Evangelism; Teaching
Features: Bible Stories; Paraphrase Scripture
Hali: Approved
Hati ni miongozo ya kimsingi ya kutafsiri na kurekodi katika lugha zingine. Yanafaa kurekebishwa inavyohitajika ili kuzifanya zieleweke na kufaa kwa kila utamaduni na lugha tofauti. Baadhi ya maneno na dhana zinazotumiwa zinaweza kuhitaji maelezo zaidi au hata kubadilishwa au kuachwa kabisa.
Maandishi ya Hati
Mara tu Yesu alipokwisha kubatizwa, Roho Mtakatifu alimwongoza Yesu nyikani, huko alifunga siku arobaini mchana na usiku. kisha Shetani alifika kumjaribu Yesu ili atende dhambi.
Shetani alimjaribu Yesu akisema; "Kama wewe ni mwana wa Mungu yaamuru mawe haya yawe mikate upate kula".
Yesu akajibu; "Imeandikwa katika neno la Mungu, watu hawahitaji mkate pekee ili wapate kuishi, bali wanahitaji kila neno linalosemwa na Mungu".
Kisha Shetani alimchukua Yesu mpaka juu ya mnara wa hekalu na kumwambia; "Kama wewe ni Mwana wa Mungu jirushe mwenyewe chini, kwa vile imeandikwa, Mungu atakuagizia malaika wake wakuchukue ili usijigonge mguu wako katika jiwe".
Lakini Yesu alimjibu Shetani kwa kunukuu Maandiko akisema; " Katika neno la Mungu, anaagiza watu wake, usimjaribu Bwana Mungu wako".
Kisha Shetani alimwonyesha Yesu falme zote za ulimwengu na fahari zake zote na akasema; "Nitakupa hivi vyote iwapo utanisujudia na kuniabudu mimi".
Yesu akajibu; ondoka kwangu Shetani! Katika neno la Mungu ameagiza, "Mwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia Yeye peke yake".
Yesu hakujitia chini ya majaribu ya Shetani, hivyo Shetani aliondoka akamwacha. kisha malaika walikuja na kumhudumia Yesu.